
ENDELEA............ Mama alinisogelea karibu na kuniambia. "Onesha tabasamu Olivia au kunatatizo!?" "Ndio mama tena sio dogo" "Tatizo gani!?" "Twende tukaongelee pembeni!" Mama alinishika mkono tukaelekea pembezoni kidogo tukiacha ndugu wakicheka na kufurahi pamoja huku wakicheza. "Ayaa tumeshafika kuna tatizo gani!?" "Mama huko kazini nimekutana na shida" "Shida gani!?" "Boss kaniambia kama nataka kazi sitakiwi kuolewa kwa sasa ivi" "Nini wewe!?" "Ndivyo alivyoniambia" "Kwanini usiolewe? na tangu lini mtu akapangiwa maswala yake binafsi?" "Hata mimi nashindwa kuelewa kwakweli, kaniambia kitengo alichonipa hakifai kwa sasa kufanya kazi nikiwa ndani ya ndoa na tena amenipa siku moja tu ya kufikiria na ikifika kesho
0 Comments