
. ILIPOISHIA..... Kabla Onesmo hajachukua hatua yoyote, alihisi kama miale ya umeme ikimpiga shingoni. Giza likatanda usoni kwake huku mwili wake ukilegea. Akaanguka chini kama mzigo, hakujua nini kimeendelea Je, mwanamke huyu ni nani? Katoka wapi? Anataka nini? Kwa nini? SASA ENDELEA... Asubuhi majira ya saa tatu, mwangaza wa jua ulipenya kupitia pazia za dirisha ukamchoma Onesmo usoni. Taratibu alifumbua macho yake, alihisi kichwa kuzunguuka na macho yake yakiwa mazito. Alikuwa amelala kitandani tena akiwa amefunikwa vizuri. Mara kuna sauti ya kike ikawa inaita mlangoni. “Onesmo… Onesmo, amka. Nimekuletea kifungua kinywa.” Onesmo aliinuka akajitazama tena. Yuko kitandani chumbani kwake akiwa
0 Comments