
ILIPOISHIA..... Tayari moyo wa kijana ulianza kupiga kwa kasi ya matamanio, kama vile moyo wa Madam sandra unavyopiga kwa kasi baada ya kupokea picha ile yenye ujumbe wenye utata. Mioyo hii miwili mmoja wa hofu, mwingine wa hisia za mapenzi. SASA ENDELEA.... Madam Sandra aliendelea kuitazama ile picha aliyokabidhiwa na yule mtoto asiyemfahamu. Alikuwa bado hajapata majibu. Macho yake yalikuwa yamejaa mshituko, na moyoni wingu zito la hofu lilikuwa linamzonga. Aliishika ile picha kwa vidole vyake vya upole, akaipindua na kusoma tena yale maandishi "Yuko wapi?" Alijikuta akitetemeka kwa hofu. Mapigo ya moyo wake yalikuwa kama ngoma ya vita kwenye
0 Comments