
Sikku zilikatika hatimaye mwezi ukayoyoma, muda wote huo Dorini na Frank waliishi kwa kuteseka sana, kula yao tabu lala yao ndiyo utawahurumia kabisa. Muda wote makazi yao yalikuwa ni yaleyale kwenye dampo, sehemu ambayo karibu takataka za mji mzima zilitupwa hapo na kama ujuavyo harufu inayo patikana kwenye dampo ilivyo mbaya, hapo ndipo watoto hawa walijikuta wakipageuza kuwa maskani yao. Si Dorini wala Frank wote wamekonda wamebaki mifupa tuu, yaani aliyewahi kuwaona mwezi mmoja nyuma na angewaona leo hangeweza kuamini kama watoto wale ndiyo hawa, yaani wamechakaa hawatamaniki, weusi tii waliojaa masizi ya uchafu mwili mzima. Chawa, kunguni, viroboto na
0 Comments