
Wale wanawake majirani hawakuweza kujibu Chochote walitoka kimya, Fina alikuwa anacheka ile kinafiki, haijulikani kwanini afanye hivyo Ray alibaki akiwa na Nasma pale ndani hata hivyo alimtazama kwa mshangao bila kuongea chochote halafu akainuka, Ray akajua hapo kuna tatizo Ray alitoka hadi nje ya chumba akatembea mpaka getini kisha akamkuta Karimu akiwa anaongea na simu pale nje. Alimsubiri akamaliza kuongea na simu "Karimu" Aliita Ray "Ee" "Nambie ukweli, kipi kilichotokea" "Mh daah" Karim aliguna kwanza huku akionyesha tabasamu Fulani hivi "Broo" Alisema Karimu "Nambie mzee mbona unaguna mke wangu kapigwa na nani mbona sielewi?" "Hama Hapa unapoishi Bro, la sivyo
0 Comments