
" Uko wapi? " Nipo nyumbani. " Nataka kuonana na wewe nina matatizo rafiki yangu. " Sawa niambie uko wapi nikufuate? " Natoka nyumbani kwake Maxwell . " Nitakuwa hapo baada ya dakika chache nisubiri hapohapo. " Sawa. Lina alisimama kumsubiri huku akiwa na hasira na Stephen. " Nitahakikisha nafanya juu chini kupanua maisha yangu siwezi kuvumilia hizi dharau. Baada ya dakika kadhaa kuna gari nyekundu ilifika na kusimama mbele yake. Lina alikuwa akiangalia kwa makini, mara kioo cha gari kiliteremshwa na Mishely ajachungulia. " Lina fungua mlango uingie. " Mishely ni wewe? Aliuliza lina kwa mshangao huku alifungua mlango
0 Comments