
Wakati anatoka chooni, alivutwa kwenye giza na mtu. "Wewe ni nani? Kwanini unanishika hivi bila ruksa yangu? Na unataka nini kutoka kwangu?" Mira alimsukuma yule mwanaume. "Kwahiyo yule ndo bwana ako mpya?” aliuliza yule mwanaume, sauti yake ikiwa imejaa hasira. "Joel..." aliita Mira kwa mshangao. "Ndiyo, ni mimi, hujakosea hata kidogo. Au ulidhani nimekufa?" Joel alimvuta Mira akamkumbatia. Joel, acha bhana, ngoja niende, nitakupigia baadaye, Mira aliitoa mikono ya Joel kwenye kiuno chake. "Nakuacha uondoke, ila nakupa onyo ole wako usinitafute, nitakuharibia kwa huyo boya wako. Nadhani unanijua vizuri," Joel alimtishia Mira. "Najua siwezi kukuangusha, nitakutafuta tu," Mira alimkiss Joel
0 Comments