
GENERAL alinituliza hapo na kunitoa kwenye hali niliyokuwa nayo, kisha tulianza kupiga story mbali mbali kutuhusu sisi wenyewe, kisha nilikumbuka na kumuambia: "Hayasasa nipe zawadi yangu uliyoniambia umeniandalia" "Ooh! nikweli ngoja nikupe mpenzi wangu, unajua ulinivuruga ulivyokuja, ulikuwa unahali mbaya sana, sipendi kuona ukilia mpenzi sipendi mtu yeyote akuumize sawa? "Asante mpenzi wangu " Kisha alienda kwenye gari na kuja na kimfuko kidogo kizuri, ndani kuna box nzuri ya zawadi, kisha alinipa hako kamfuko na kuniambia: "Haya fungua mpenzi" Nilifungua kile kifuko na kutoa box iliyokuwepo ndani yake, kisha nikatoa na kuifungua ndani ya box, nilikuta mkufu mzuri wa gold
0 Comments