
Mama akawa anagomba weee, kunipiga ndo alikua hawezi kabisa😅, Sababu nilikua mtoto pekee alie barikiwa na Mungu. Kuona sipigwi na Maneno ya mama nishayazoea nikawa nazidi kuchochea ukorofi, mpaka namaliza Form hali ikawa ni tete. Matokeo yalipotoka nikawa nimepata division 4 ile ya mwisho kabisa😫, Na apo Form 2 nilipataga Division 1. Mama akawa analalamika atanipeleka wapi coz kwa maksi zile nilizopata sikupata nafasi ya kwenda chuo wala Form 5. "Hapana! Hapa kwangu sitaki kukuona, bora uende kwa mjomba wako" Alisisitiza Mama "Mjomba? Unataka nikafe uko"🤨 "Uende uko mjomba wako akakunyooshe vizuri! Umenishinda tabia" "Mama na wewe, Mimi si nimebadilika
0 Comments