
. Leyna, Leyna... Abisai alimuita Leyna aligeuka akamuangalia kisha akakata mwendo. Abisal alikazana kutembea mpaka akamfukia. "Nilikwambia twende kwenye gari huku unaenda wapi? Sitaki, sihitaji chochote kutoka kwako niache na maisha yangu Abisal. Hiyo itakuwa ngumu na usitake tujaze watu hapa naomba twende tukaongee tukiwa kwenye gari. Leyna alijikuta akimuangalia kwa hasira huku machozi yakimtoka. Katika siku zote leo umenidhalilisha kupita kiasi, Abisai kama upendo wako kwangu upo hivi basi mimi siwezi. Kwa mara ya kwanza Abisai alijihisi mwenye hatia, aliona maumivu ya Leyna. Tafadhali mamy twende tukaongee. Akiongea kwa upole Leyna akajikuta anakubali kumfuata wakaenda alipoacha gari, walipanda na
0 Comments