
Romex mwanangu mbona unataka kutibua nguo, familia ya kina Lilian unatuamini sana na ukizingatia tumeshsungana kibiashara kuna mambo tuna share pamoja. Kwanini unataka kuuvunja huu muungano mwanangu. Aliongea mama Romex huku machozi yakitaka kumtoka. Hali ilikuwa ngumu kwa Romex alikuwa kasimama katikati yao, moyo wake ukidinda kwa kasi lakini bado akiendelea kushikilia msimamo wake hakutaka kabisa kumuondoa Salsa kwenye maisha yake. "Baba, mama... naomba msinihukumu kwa hasira. Nimefanya makosa ndio. Lakini huu sio wakati wa kuniona kama adui yenu. Niko tayari kubeba majukumu ya matokeo ya matendo yangu, ila siwezi kuishi maisha ya uongo kwa sababu ya heshima ya kifamilia.
0 Comments