
Nilishtuka baada ya yule jamaa kuwapiga wale watu watatu kipigo kizito. Namna alivyopigana nao ili onekana anauwezo mkubwa wa ujuzi wa mapigano. Basi baada ya kuwaangusha wote chini aliinuka nakuvua kofia yako huwezi aminI ni KELVIN..... Nakubaki namshangaa sana kwa kuwa hata sikuelewa kafikaje hapa lakini hakuwa na muda wa kujieleza alinipitisha njia za panya sekunde chake nipo kwake. Alinisogelea kwa hasira huku kanitolea macho " nilikwambiya nini Lucy? " Nisitoke nje " " Na umefanya nini sasa" Kwa aibu" samahani kuna kitu nilitaka nikuagize" " Si ungesubiri nirudi? " " Nakuahidi sitarudia" " Haya kapike uko " Kisha akaondoka
0 Comments