
Majira ya saa tatu na nusu asubuhi. Ukumbi wa kusubiri uliokuwa ndani ya Hospitali ya Mji Mkuu ulikuwa umetulia mashine zikiunguruma kwa mbali, wauguzi wakipita kwa haraka huku na kule. Ndani ya ofisi ya juu kabisa ghorofa ya nne, kiti cha ngozi cha rangi ya kahawia kiligeuzwa kuelekea dirishani, kikiwa kimebeba mtu mmoja mwenye mamlaka ya mwisho ya ajira Dkt. David Alijulikana kwa usomi wake, aliheshimika kwa umahiri wake, lakini wachache sana walijua siri ya ajira hospitalini hapo kitanda chake ndicho kilikuwa sehemu ya mahojiano yasiyo rasmi.Na aliamini kuwa sehemu pekee ambayo mtu atapata kazi kwake hususani jinsia ya ke
0 Comments