
Jimmy alirudi nyumbani kwao akiwa hana raha hakutaka kuongea chochote na Maria alienda kukaa chumbani . Baada ya muda Maria alifika chumbani. " Jamani mpenzi nilikuwa nakusubiri sebleni nikajua utakuja kumbe upo huku umelala. " Maria naomba uniachie leo sipo sawa kabisa. " Haupo sawa una umwa ? " Hapana. " Kumbe una nini? " Wewe niache tu. " Sasa usiponiambia shida zako mimi ninaishi na wewe hapa ndani utamwambia nani mwingine? Jimmy hakujibu chochote aligeukia upande mwingine. " Basi kama hutaki kusema nilikuwa nina shida yangu hapa. " Shida gani? " Mama alikuwa anaomba pesa kiasi kama cha laki
0 Comments