
Walipofika mlango wa kuingilia ukumbi, mlango mkubwa wa kioo ulifunguliwa kwa heshima. Ndani kulikuwa kumepambwa kwa mapambo meupe na ya dhahabu, maua, taa za kung'aa, na meza zilizopangwa kwa umaridadi wa hali ya Juu. Prisca alihisi miguu ikitetemeka. Aliinama. kidogo kuangalia pete iliyokuwa kidoleni mwake. "Ni kweli haya yananitokea mimi? Alijisemea. Jimmy alimsogeza karibu na kumnong'oneza, "Leo ni siku ya furaha Wewe ndiye malkia wa usiku huu naomba usiniangushe. Wakaingia ukumbini Watu walishangilia, wengine wakapiga makofi, na wengine waliwaangalia kwa mshangao. Kamera ziliwaka kila kona. Prisca kijasho kilimtoka alikuwa akitetemeka kwa hofu lile jambo lilikuwa kubwa kuliko alivyokuwa amejichukulia. Alimwangalia
0 Comments