
Basi bana maisha yakawa yanaendelea kwenda kama kawaida, na mume wangu aliendelea kunifanya kuwa mwanamke wa thamani na mwanamke bora sana kwake, hakuyumbishwa na maneno ya mtu yoyote Yule, maana yeye ndio aliamua kunipenda na hakuna mtu mwingine yoyote Yule ambae anaweza kuuvunja huo upendo ambao alikuwa nao kwangu… Siku moja nilirudi nyumban mapema baada ya kupigiwa simu na mwalimu wa mwanangu kuwa mwanangu anaumwa, nilipofika nyumban, nikamkuta mama yangu mkwe, nikamkuta pamoja na kaka mmoja wa mume wangu, alikuwa mkubwa sana kwa mume wangu, inawezekana hata akawa marika yangu, ila alikuwa mlevi balaa, pamoja na yule binamu wa mume
0 Comments