
Mwenyekiti ilibidi awatulize na baadae tulikaa kikao na mtu wa kwanza kuongea alikuwa ni Alex. "Mwenyekiti waambie wanipe mwanangu mimi niondoke" "Huna mtoto hapa wewe ivi huelewi au!?' Mzoa taka aliongea kwa mara nyingine na mwenyekiti aliamua kuniuliza mimi ambae ni mama wa mtoto. "Binti emu tuambie ukweli ili tuwezi kulitatua hili baba wa mtoto hapa ni yupi kati ya hawa wawili...!?" Baada ya mwenyekiti kuniuliza sikutaka kumficha Alex na ukizingatia hakuwa mme wangu kwa wakati huo. "Baba wa mtoto ni Damian na sio huyu Mwenyekiti" niliongea nikiwa na maana kuwa Alex sio baba wa mtoto wangu. Baada ya mimi
0 Comments