
Wakati huo jua lilikuwa linapotea juu ya anga na giza lilichukua nafasi yake Wakiwa kwenye gari kimnya kilitawala na safari hii Victor waliendesha gari kistaarabu. " Suzan najua unaniona mtu mwenye roho ya ajabu ila nafanya haya yote kwasababu nakupenda. " Mmmmh.... Suzan aliishia kuguna. " Mbona unaguna? " Sijawahi kuona mapenzi ya aina hii, mapenzi ya kulazimisha haupo romantic unalazimishwa mambo unafikiri mimi naweza kukupenda kwa moyo wangu wote kwa haya unavyomfanyia kweli? Victor alitabasamu " Mimi najua umeshanipenda tangia siku nyingi . " Sio kweli na kama unahisi nilikubusu kwasababu ya upendo basi unajidanganya ule ulikuwa ni mchezo
0 Comments