
"Mama yake Angela kalazwa kama nikienda kazini itakuwa ngumu kwangu kupata ruhusa...." Mama alinitazama kwa msisitizo hakusema chochote aliendelea na kazi zake Baada ya kumaliza kuandaa chai nilielekea hospital nilifahamu fika Angela kalala hospital hivyo asingeweza kuandaa chai kwa ajili ya Mama yake "ni muda wa wewe kumfahamu Baba yako.....nasema hivi kwa sababu sina uhakika wa kuiona kesho.." "Mama.... maneno gani hayo una zungumza..." "Baba yako yupo hai...tena ana maisha mazuri tu, sitaki uendelee kuteseka naomba uende kwa Baba yako.... Angela, Baba yako hawezi kukukataa kwa sababu amekuwa akikuulizia sana japo Mimi nilikuwa na mkwepa" Ni mazungumzo niliyoyasikia kabla sijaingia
0 Comments