MAPENZI YA KUKOMOANA PART: 01

MAPENZI YA KUKOMOANA  PART: 01

Kwa majina naitwa Cathe naomba twende wote. Ilikuwa siku ya jumamosi mida kama ya saa 3 hivi za asubuhu huku nikiwa naamka kitandani ndipo simu yangu ilipoita.. Taratibu huku nikiwa najinyoosha, nilichukua simu ile kuona nani anapiga ndipo nilipokuta ni rafiki yangu Dicky ambaye mda mwingi alikuwa ananitongoza lakini kiukweli sikuwahi kumuelewa kabisa . Nilipokea simu yake kisha tukaanza kuzungumza, "Heloo.." nilitamka "Heloo mrembo nimekumis kweli " Dicky alitamka. "Mhh..uongo mbona ulikuwa hunitafuti?" Nilimuuliza. "Mambo yalikuwa mengi kidogo vipi za siku?" "Ni nzuri, nisaidie hata vocha basi.." nilimwambia. "Ohoo haina shida nakutumia tukimaliza kuongea ." ",Asante.." "Vipi upo nyumbani?" Aliniuliza.

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments