
aliniambia baada ya kuona najiandaa taratibu sana, yaani swala la kujiandaa taratibu ilikua ni jadi yangu hata niseme niwahi vipi bado nitakua wa mwisho tu mmmh sijui nipoje yaani, upole wangu ulikua wa sura mpaka matendo nayo yalikua ya pole pole. "Hehehehe nisiongee sana nitaonekana nna kamdomo rafiki angu mwingine wa kuitwa Cammilla alidakia "Heee jamani msinivamie kwa maneno sasa mwenzenu nitajisikia vibaya, hata hivyo. nimemaliza tunaweza kuondoka nilijitetea. Mlango wa chumba cha hostel ulifunguliwa aliingia mwanadada mwingine huyu aliitwal Petronida alikua anakaa chumba cha jirani na chetu. "Vipenzi vyangu mwenye shughuli yake yupo tayari, pia tumerequest bolt tufanye kwenda
0 Comments