
alizunguukwa na wapangaji wote waliokuwepo wakitaka awaeleze kuhusu Sele, “hivi anaongea kabisa, halafu anacheka?” aisha alidakia “jamani Sele ni mwanaume mzuri tu kama walivyo wanaume wote, yaani sijui nisemeje ni binadamu kabisa!” alisema ester sasa alishachoka kufanya mahojiano ambayo kwa uono wake yeye haukuwa na kichwa wala miguu, “haya tuambie mlikula nini, kawhiyo Sele pia anakula kabisa!” aliuliza mama Mwajuma! “hahahaha jamani mama, eti anakula, kwahiyo bado mnaamini Sele ni Zimwi, sijui jini huko..” alisema ester akiingia ndani “na mizigo yote hii mwanangu umemaliza mshahara wako huko!” alisema mama mwajuma “hapo vitu vingi kaninunulia Sele” alisema Ester sasa akiangalia hotpot
0 Comments