
pembeni na kisha akamsogelea Sele pale kwenye sofa na kumshika bega, “Sele, naomba kwanza nisamehe sana ila sina namna nyingine isipokuwa hii” alisema akianza Alimsimulia Sele kuhusu historia yake ya maisha, elimu yake na mapenzi na kisha akamsimulia kuhusu mama Mwajuma na hadithi nyingine ambazo hakuona umuhimu wa kuzificha “ mama Alikuja kutafuta maisha Dar miaka wakati huo aliniacha na bibi, kwa uhalisi mama alipata ujauzito akiwa darasa la saba, na mara baada ya kujifungua na mimi kuacha kunyonya ndio akaja huku Dar, alikuwa kila mwaka anakuja na kuniletea nguo na pesa za matumizi na hatimaye nikamaliza darasa la saba
0 Comments