
Chakula chake cha usiku nilikuwa nakipikia nyumbani kule mgawahani kwetu hakuna hata umeme pale ni spesheli kwa chakula cha asubuhi na mchana tu😍😍 Basi bwana nilimwelekeza akaniambia anakujaa🙈🙈 ilibidi sasa nianze kumpakulia msosi wake kwenye hotpot nzuri mteja ni mfalme bwana😍 Ile juice niliitia kwenye kopo fulani hivi naloekea maji yangu ya chuo🙈🙈ni zuri😍😍 Hemed alifika karibia na kwetu akanipigia.. Nilimuomba asije na gari yake mpaka nyumbani majirani wataanza kutudisi hahahaa mi naogopa🙈🙈 aliegesha gari kwa mbali kidogo kisha akatembea mpaka kwetu🙈 Nilimkaribishia nje kulikuwepo na kiti pale akakaa nikamtolea chakula chake nilikuwa nimekifungasha vizuri akanishukuru baada ya hapo akatutakia
0 Comments