
Sehemu ya 07 Nesi Tina alielekea mochwari kwa haraka sana. Alipofungua mlango, alishtuka kupita kiasi. Hakuamini alichokiona, akapiga kelele: "Haaaaaa!!!" Alimuona Daktari Mery akiwa ameshika kipande cha nyama ya maiti na kukitumbukiza mdomoni. Sauti ile ya mshangao ikamfikia Mery, na mara moja akashituka; kisu alichokishika kikaanguka chini. Machoni mwake pakatoa mwanga mkali uliomuelekea moja kwa moja Tina, na kumfanya ahisi kuungua usoni. Akili zikamrudia haraka, akaamua kukimbia kabla hajauawa. Mbio zake zilimfikisha hadi kwenye kikao alichotumwa kumuita Mery. Alifika pale akiwa anahema kwa kasi, kijasho chembamba kikimtoka. Mganga mkuu akamuuliza: "Vipi? Tumekutuma kumuita Mery mbona unarudi
0 Comments