
Alipozaliwa alipewa jina la Agness lakini taratibu lilibadilika na kuwa Laviollete La Chapelle wengne wakimwita kwa kifup Lavio na wengne wakimwita LALACHA Mwili wake uliojaa vizuri sio kwa afya bali shughuli pevu ya kusonga sufuria ya ugali katika mgahawa mdogo wa mama yake,sura yake ilipambwa na mikunjo ya hasira kwenye paji la uso hyo ikimaanisha hataki mchezo awapo kazini,ilikuwa si jambo la kushangaza kumkuta akiwa amekabana mashati na wateja wakorofi bila kuogopa jinsia zao na wakati mwingne ilifikia hatua ya kupigana kabisa. Licha ya yote hayo Lavio alikuwa mchapa kazi hasa hakuwa legelege hata kidogo hicho kiliwavutia wateja wengi sana.
0 Comments