
Baada ya kugundua kuwa Vanessa ni mwanamke mwenye elimu yake nzuri Damiani alikuwa mtu mwenye mawazo sana , alikosa usingizi akimfikiria. Kuna muda alitamani kukaa na Vanessa waongee kwa kina lakini aliona ni mapema sana na anaweza akamuuliza Vanessa akaruka na asimwambie ukweli. " Nahitaji kuendelea kufanya uchunguzi zaidi. Kesho yake asubuhi Vanessa aliamua na kuandaa kifungua kinywa lakini Damiani hakutoka chumbani kwake. " Huyu mtu mpaka sasa saa tatu hii hajatoka huko chumbani itakuwa kuna shida acha nikamuone. Alipandisha ngazi na kwenda kusimama kwenye mlango wa chumba cha Damiani , aligonga mara mbili mlango ukafunguliwa. " Habari za asubuhi
0 Comments