
Maisha ya ndoa baina ya Zayn na Leila yalikuwa yasiyo hata na chembe ya furaha. Ilikua ni ndoa kwa jina tu. Zayn alikua haonekani nyumbani, hata Jumapili ambazo kwa kawaida watu hutumia kukaa na familia, yeye alikuwa sehemu isiyojulikana. Na kama Akirudi basi hujifungia chumbani kwake, na siku nyingine hakuonekana kabisa🤦♀️. Leila alizoea ukimya. Alizoea upweke na kutokuhesabiwa kama mtu wa muhimu. Mlinzi wa getini ndiye aliyebaki kama mtu pekee ambae alikua akiongea nae. Hata hivyo, hakuacha kwenda Coco Beach kuuza madafu kama zamani. Ile sehemu ndo ilimpa amani na pia ni sehemu ya kupatia hela ya kuendesha maisha yake.
0 Comments