
Ilikuwa ni Jumamosi ambayo Mama Bry aliamka furaha tele baada ya mwanae wa kiume, Bryton ambaye anasoma huko Texas nchini Marekani kumpigia simu kwa njia ya Whatsapp video na kumtaarifu kwamba anakuja nyumbani, yupo uwanja wa ndege nchini Marekani na sio muda ataianza Safari. Mama Bry alifurahi sana na kuamua kuandaa hafla fupi (🎉 party) kwa ajili ya mwanae. Majira ya saa tisa alasiri, Bryton aliwasili uwanja wa ndege wa Mwl. Julius Nyerere na kuchukua Taxi ambayo ilimpeleka moja kwa moja mpaka nyumbani. Alipokelewa kwa shangwe kubwa huku ndugu zake waliokuwepo hapo nyumbani wakimkumbatia Bryton kwa furaha sana. "Oooh karibu
0 Comments