
Mara zote nimekuwa nikitamani kuwa na ndoa yenye amani na furaha. Sijawahi kuwa aina ya mwanamke mtukutu hata kidogo, na utukutu siuwezi kabisa. Kila mmoja anapoona utajiri wa mume wangu anatamani angekuwa ni yeye afurahie hizo mali. Lakini mhusika sitaki hata kumuona huyu mwanaume ambaye yamkini wengi wanamtamani. Hii ni kawaida kabisa kwa mila na desturi zetu ama tamaduni zetu. Kusema unaachana na mwanaume tajiri kila mmoja angekuona kama punguwani ama hamnazo. Kila mmoja angeamini furaha ni katika utajiri na majumba yetu, lakini asiamini furaha na amani katika kidogo ama kikubwa mlicho nacho. Nilikuwa sasa nimeshafikia upande wa pili. Awali
0 Comments