
Nilifunga geti nikarudi ndani nimeshika ile juice, nikawa nawaza hivii ,zakia mbona amekasirika kama kwahiyo alitaka ofisini tuwe tunaitana tunapiga story mpaka basii auu?? Mtoto mpuuzi sana huyu yaan ni mpuuzi mpaka mwisho afu kashenzi kweli , niliiweka ile juice ndani ya friji mi napenda sana juice ya tende mnoo ila iwe ya baridi ye alinipa haina ubaridii Mpenzi wangu akanipigia simu upo home nikamwambia nitakwenda wapi mimiii!! Akasema sawa nakuletea wageni sawa nikasema sawa Zilipita kama dakika hamsini , Nikasikia kuna gari inaingia , sikuamini nilimuona Alex mama yake na baba yake afu na inno wanakuja kwangu moyo ulinishtuka
0 Comments