
Nikamwambia mama sasa kwanini hukuwahi kuniambia mama yangu??, akanambia kwanini nikuambie mambo mabaya kama hayoo salma , nimesema leo kwa sababu ilitakiwa niseme Nikamwambia mama nisamehe nilikuwa nakujibu vibaya kipindi kile akasema usijali ni kwenye Ukuaji m hiyo kawaida ... "Mama naomba nikuulize kitu " "Kitu gani tena salma??" "Umesema baba aliondoka wakati una mimba yangu na subira jee?? Inamaana baba alirudi??" "Mhu yaan wewe umewaza ninii??" "Nataka tu kujua mama!" "Baada ya miaka sijui 8 mana wewe ulikua na mkubwa kabisa hadi nilisha sahau kabisa kuhusu maradhi yako ndio baba yako alirudi , na kipindi hicho ndoa ilikuwa inaheshimiwa
0 Comments