
Zilisikika kelele za watu waliokuwa wakisema.. "Mwiziiii...mwiziiiii ..mwiziiiiii" Jamani mwiziiii" Mida hiyo mimi nilikuwa zangu bafuni naoga.. jamani kaiba wapi tena huyoo aah haya maisha ya uswahilini bwana kila siku kuna jipya.., nilichukua ka upande kangu ka khanga nikajiweka mwilini kelele zile zilikuwa zinasogea kwa kasi kuja upande huu wa kwetu .. Ilikuwa mida kama ya saa 4 hivi usiku kwenda saa tano , nimetoka zangu kibaruani kwangu mihangaiko kama unavyojua wahangaikaji tunakula kwa jasho.. nimejichokea hatari.. "Sijui kaiba wapiii" hapo nawaza nitoke nikaangalie maana kelele zillikuwa zinakuja mtaani kwetu..basi ile nafungua mlango nitoke bafuni nilishtuka mlango umesukumwa kwa nguvu
0 Comments