
Basi bwana boda akanirudisha mpaka nyumbani .....nikifika nikamkuta mama lulu kakaa na Robby pale nje wanapunga upepo nikaenda pale alipokuwa mama lulu ....nikapiga goti mama mzigo huu hapa....kwa sisi tuliotokea bush kupiga goti wakati mkubwa amekaa ni kitu cha kawaida ....mmmh huyu mtoto ana heshima jamani sijawahi kuona....mama lulu akaongea ....daaah nikaona aibu😌....huyu anafaa kabisa kuwa mke wa fulani huyu.....robby aliongea huku akiwa ananikazia macho....akanikonyeza 🤣 bas nikaangalia chini.......mmh huyu hana aibu hata kwa mama yake......nikawaza....wakat huo mama lulu alikuwa akimnyoosha robby miguu..... huo mzigo ni kwaajili yako mwanangu .....mama lulu alinambia .....wa kwangu mama?.....nilimuuliza kwa kushangaa...ndiyo nenda ndani ukaangalie
0 Comments