
Nilimgeukia Selim na kumwambia "mh nipe umbea kimetokea nn?" "Na ukaniamini kuwa nina umbea" "Selim umeanza sema bwana " "Niseme nini wakati nimeshinda ndani umbea ningeutoa wapi" "Kwahiyo ulivyokuwa unaniambia unaumbea ?'" "Nilitaka tupate dhambi wote ,we unaweza kwenda motoni peke yako?" "Bata wewe" " Paka wewe" tulikaa seblen kwa mda mrefu kisha tukaingia chumbani na kulala ,kesho yake niliamka mapema na kwenda jikon nikaanda chai kisha nikaweka mezani . Mara mlango ukagongwa nikaenda kufungua nashangaa Nasra ,nilimuangalia juu chini na kumuuliza "Kuna msiba Au mbona asubuhi asubuhi " Alijichekesha nakujibu "hamna kila kitu kiko sawa ila nimekuja kukusalimia tu"
0 Comments