PAKA WA MAMA KIZIBO SEHEMU YA SABA

PAKA WA MAMA KIZIBO  SEHEMU YA SABA

Baada ya bwana Bakari kuachwa hotelini hakutoka nje ya chumba chake. Muda mwingi aliumaliza akiwa amaangalia vipindi kwenye televisheni kubwa ya kisasa iliyokuwa imeunganishwa na ving'amuzi vinne tofauti. Ilipofika saa mbili usiku aliitisha chakula na matunda vikaletwa na mhudumu katika chumba chake. Alipomaliza kula akaenda kuoga tayari kwa kwenda kulala. Wakati anaweka nguo zake kwenye kabati simu yake ikaita. "Mimi ni Jah Sam naongea. Naomba ujiandae, kesho alfajiri nitakupitia kuna sehemu nimeambiwa nikupeleke" Samwel Rweikiza aliongea taratibu kama anayekusudia kila neno liingie barabara kwenye masikio ya Bakari. Kabla Bakari hajauliza wala kusema chochote simu ikakata. Mwanzoni Bakari alidhani ni tatizo

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments