
Apite mbele kabla sijamfuata, Nilitulia ili nione ni nani atakayepita mbele sababu najua barua niliandika mimi na kumpatia Side apeleke kwa Tina, Mwalimu alipoona hakuna anayepita mbele alikuja pale ambapo tumepanga mstari akamchukuwa mwanafunzi ambaye alikuwa anafahamiana na Side akampeleka pale mbele, Kisha akamwambia wewe ndio ulipeleka barua kwa Tina bas katuletee aliyeandika hii barua, Yule mwanafunzi alikuja pale tuliposimama mimi na Side, Niliogopa nikajua ni mimi nafuatwa cha ajabu yule mwanafunzi alimshika Side na kuelekea naye pale mbele. Mwalimu alimwambia Side chukuwa hii barua na uisome kwa sauti, Side alianza kuisoma ile barua hadharani kila mwanafunzi anasikiliza. KWAKO MPENDWA
0 Comments