POOR RICHMAN* (Alijifanya amefirisika na Kuwa Masikini ili kuwajua wanafiki kwenye Maisha Yake) Sehemu Ya 8

POOR RICHMAN*  (Alijifanya amefirisika na Kuwa Masikini ili kuwajua wanafiki kwenye Maisha Yake)  Sehemu Ya 8

"Keivo najua Wewe ni Sugu hivyo vidonda utajikaza! Sitaki tulaze Damu, kuna fala Usiku Huu tunamvamia tunaenda kupora Pesa na nina maswali mengi ya kumuuliza pia!" Yalikuwa maneno ya kujiamini ya Jovin Huku akiwa anaonekana yupo Tayari kumwaga ubongo Wa Mtu na ile Bastola. Basi ni kweli Usiku kwa Usiku wawili wale walikodi boda mpaka mtaa karibia Wa Nne kutoka pale walipo!. Ilikuwa ni kwenye Moja ya nyumba nzuri kabisa na ya kifahari!. Jovin aligonga geti!!. "Oya nani!!? " Basi Jovin alisikia Sauti ya kukoroma upande Wa ndani, bila shaka ilikuwa Sauti ya Mlinzi. "Ni Mimi Maria naomba fungua mlango!"

Soma zaidi

Post a Comment

0 Comments