
Baada ya Nesi Tina kumchoma sindano ya sumu mgonjwa, akamwambia muuguzaji "haya nishamtibia mgonjwa wako 'una lingine??, hapana nesi nashukuru sana. Tina aligeuka kurudi zake ofisini ,bado aliendelea kuuwazia usiku ule ulioonekana mfupi lakini ulikua na maajabu mengi kwake, alikumbuka pale alipozishambulia nyama pasi kujua ni za binaadamu hadi alipomaliza, akasisimkwa mwili 'mh zilikua tamu, ndio maana Dr mery siku ile alikwenda mochwari kula nyama ya binadamu ila yeye anakula zisizopikwa hiv zina utamu kweli????. Ni mambo aliyokua akiyawaza Nesi Tina .muda ulifika kuwapa wagonjwa dawa, alinyanyuka kurudi tena wodini, alianza kupita kitanda hadi kitanda, alipofika kwa yule mgonjwa aliemchoma
0 Comments