
JUMAPILI KAMA JUMAPILI Asubuhi saa kumi na mbili kasoro alishtuka usingizini mtoto, Nasma, safari ya kwenda Singida ilikuwa imeshaahirishwa kabisa kutokana na kwamba binti hakutaka kuondoka wakati bado Ray yupo, alijitia moyo “Ray akiondoka hivi, na mimi ninaondoka” aliwaza binti. Alishuka kitandani, yaani cha kwanza kushuka ni lile limfuko la zawadi, aliliotoa na kuzimimina zote kitandani, kisha akaangalia zile shanga akatabasamu, “Sasa mimi hizi naweza kuvaa jamani, kwanini aninunulie hizi, mmmh” alisema kwa furaha huku akizitazama, halafu akaziweka kitandani na kuweza kuchukua gauni. Alijifungua khanga yake halafu akavaa gauni lile, halafu akakuta ni fupi “Mh mbona hili fupi sasa” alifikiria
0 Comments