
Ikiwa ni saa saba mchana, mjini mwanga, Ray alikuwa amesimama mbele ya duka la Tesha, lilohusika na uuzaji wa vifaa vya ujenzi. Alikuwa ameshika cocacola mkononi huku akilikwepa jua lililokuwa likiwaka japo ilikuwa ni enzi ya masika katika ukanda wa Afrika Mashariki kiujumla. Ray alikuwa anamsubiti binti afike, lakini kabla hajafika, alisikia ujumbe umeingia kwenye simu yake akakuta ni ujumbe kutoka kwa Rose “Ray asante kwa yote, kumbe umeamua kubadili kitasa” alituma binti “Ok nashukuru, nimeweza kukukwepa maana nimechekwa sana na marafiki zangu” alijibu Ray “Sawa bana, powa tu ila kosa moja tu limekusababisha ukasahau yaliyo mia?” aliuliza binti “Ndio,
0 Comments