
Mama aliikagua ile simu, hakukuta message wala simu imepigwa na Ray, kwani baada ya kuona dalili za mama kujua kilichoendelea, basi alifuta kila aina ya ushahidi ikiwa ni call history pamoja na jumbe zote walizochat. Mama alimuangalia machoni weee, binti akaona aibu, lakini alimrudishia simu yake bila kusema lolote binti akapita ndani **** BAADA YA WIKI MOJA Ilikuwa ni usiku mida ya saa nne, Nasma alikuwa amejilaza kitandani mwake, na Ray alikuwa ameketi sebuleni anaagalia TV na wazazi wake huku akiwa anatikisa miguu na simu iko mkononi. Alikuwa anajisikia kiajabu ajabu sana Mara ujumbe kwa simu yake akaufungua ni wa
0 Comments