
Siku hiyo ilikuwa ni siku mpya yenye furaha na iliyojaa matumaini makubwa kwa hao wapendanao wawili. Hasa kwa upande wa Salma aliona kuwa sio ndoto ni kweli Fariss alikuwa na nia nae ya dhati. " Naona kama masihara kila unapojaribu kukumbuka ile siku ya kwanza tulipokutana. Alisema Salma huku akimuangalia Fariss , wakati huo fariss alikuwa akiendesha gari. Fariss alitabasamu na kusema " Unazungumzia siku uliyotaka kutokea ajali ukaangusha miguu ya kuku? " Sema mboga. Unajua siku ile nilikuwa nina njaa sana nilitoka kuzunguka mitaani kusambaza sare ya shuhuri ya rafiki yangu nimefika nyumbani hakuna kitu nikapika kiugali changu kidogo
0 Comments