
Farris alienda kuchukua gari baada ya dakika kadhaa alifika na gari yake na kusimama mbele ya Salma. Salma alifungua mlango wa gari na kupanda na kukaa kwenye siti ya pembeni ya dereva. Farris aliwasha gari wakaanza safari ya kuelekea mtaa wa saba. Wakiwa njiani kila mmoja alikuwa kimnya. Salma aliamua kuvunja ukimnya kwa kusema. " Umeadimika sana hautaki kurudi uswahilini kwetu . Fariss alitabasamu kisha akasema " Hakuna ulichoniibia ningeweza je kurudi tena? Salma aliishia kucheka. " Ulisema labda uniibie moyo wangu lakini nilipokaribia kuutoa na kukukabidhi uliamua kuondoka. Waliendelea kupiga story za kuchokozana walipokaribia kufika maeneo ya kwa kina
0 Comments