
******* 👉(Ukihitaji VIPANDE VYOTE 50 Vya Stori hii Full, Nicheki WhatsApp👉 0675137453, Kule Tumeshaimaliza yote🙏) ****** "Kokorikooooooo!!!" Sauti kali ya Jogoo likiwika karibu kabisa na dirisha langu ndiyo iliyonikata usingizi, na hakuita mara moja aliita zaidi na zaidi kana kwamba ametumwa kuja kuniharibia usingizi kabisa. "Aaah makuku mengine kama yametumwa vile.." nililalamika huku nikijifunika shuka vizuri gubi gubi mpaka kichwani, leo ilikuwa ni siku ya mwisho wa juma, sikuwa na ratiba ya kwenda shuleni, siyo kwamba hakukuwa na vipindi, vilikuwepo ila tu sikuwa na mpango wa kwenda leo na hali ya hewa ilikuwa ni ya manyunyu manyunyu, mvua ikinyesha kidogo
0 Comments