
Nikiwa pale nikaanza kuhisi kama kuna mtu ananiangalia sana, ila kiukweli sikumzingatia maana kwanza sikuwa nahisi kama kuna mtu ambae ananijua eneo lile, sasa inakuwaje mpaka mtu awe ananiangalia na hanijui hata kidogo... Nikageuka ila sikumuona vzr hivyo nikapuuza zangu nikaendelea na mambo yangu, basi kuna muda akaja mkaka akakaa pemben yangu, nikashangaa namba ngeni inaingia kwenye simu yangu na kusema "upo wapi?.. Sikujibu maana nilihisi mtu kakosea namba.. Mara nikaona sms nyingine inasema "sophy upo wapi?.. Nikaona sasa huyu ananijua.. Nikauliza "nani mwenzangu?.... "Jibu kwanza swali kabla ya kuuliza swali lingine, nakuuliza upo wapi?.. "Siwez kumjibu mtu nisie mjua
0 Comments