
Mama Zawadi akasema, “Mimi ndiye bosi wako, nitakaye kukupea mshahara, nakuambia ufanye kitu, unabisha?” Nikasema, “Samahani, mama, sikuwa nimeelewa, mama yangu.” Akasema, “Nataka nikuone mwili wako kama huna mambo ya kishirikina kama chale au hirizi.” Nikasema, “Sawa, mama, lakini sina vitu hivyo.” Akasema, “Vua nguo sasa.” Nikatoa nguo, nikabaki uchi kabisa, kwani hata chupi sikuwa nayo. Akanitazama, akasema, “Geuka.” Nikageuka, akaangalia, kisha akasema, “Vaa nguo zako.” Nikavaa. Akasema, “Na chupi je?” Nikasema, “Sina, mama, nyumbani hawajawahi kuninunulia.” Akasema, “Umevunja ungo?” Nikasema, “Hapana, mama.” Akasema, “Umemaliza shule lini?” Nikasema, “Mwezi wa kumi mwaka jana.” (Muda huo ulikuwa mwezi wa kwanza mwaka
0 Comments