
"Alex!!! Hapana!!!! Linda alipiga kelele huku mmoja wa polisi akimfungua. Linda Alimkimbilia Alex na kuweka kichwa chake mapajani mwake. "Alex tafadhali fungua macho yako, niko hapa, nakuomba. ona nimekusamehe samahani kwa kukimbia ila amka" aliongea akimchukua huku akilia lakini alishindwa KUONGEA na alizidi kulia. "Alex!!!" Alipiga kelele na kuzimia Michael alihema kwa huzuni huku akiita gari la wagonjwa huku polisi wakiendelea kumtafuta Oscar. ***Saa chache baadaye*** Linda aliamka na kutazama pembeni yake. Kwa kweli ilionekana kuwa ngeni kwake na hapo ndipo kumbukumbu za hapo awali zilipomjia na kushtuka. "Alex, Alex yuko wapi" Alifoka na Mabel ambaye amelala aliamka na kusimama
0 Comments