
Nilishusha pumzi huku haja ndogo ikinibana kwa presha nilinyanyuka nikaomba ruhusa ya kutoka nje ili niende uwani... Huku nyuma Gerson alienda pale mbele alielekeza mwanzo hadi mwisho watu wote wakajikuta wanaelewa hadi lecture mwenyewe alipiga makofi.... Nilirudi darasani nikakuta ni muda wa mapumziko kila mtu alikuwa ananisifia wa kwenye grupu letu moyoni wangejua hata sijafanya mimi hiyo kazi 😁 .. Nilimuona Gerson yupo amekaa na rafiki yake wanakula, nikaamua niende nimfuate nikaenda kukaa pale alipo wadada waligeuka kunitazama akiwemo Penina.. Ulisema nije.... Anhaa umekuja madam Angel 😇. Jana nilijua tu hutaweza kufanya hizi hesabu ndio maana nilienda kufanya na mimi
0 Comments