
Lakini nakupenda zile zilikuwa ni hasira tu mamaa, nielewe basi,niligoma kabisa lakini hakuacha aliendelea kunisumbua, Albert kuwa muelewa basi nahitaji kwenda dukani, kumbuka naishi kwa kujitafutia heshimu kazi yangu, usinipeleke peleke, " naelewa Joy wangu, ndio maana nimerudi sikuondoka makusudi nielewe kwanza, nilipata emergence ya ghafla kwenda masomoni, niliomba muda imekuja kutoka ghafla sana, nikajipa moyo nitakupata kwenye simu, lakini hukupatikana, nilitamani ningemwagiza mtu lakini hakuna aliekuwa anakujua zaidi yangu, ikabidi niwe mvumilivu, kila nikikucheki naambiwa hupatikani, nimerudi hata wiki sina nimekuja kukutafuta Joy nielewe basi... Aliongea uku ananitizama jicho la huruma,nilimuomba anipe muda kwanza make simuelewi elewi, alinikiss nakukubali
0 Comments